Jumatano 8 Julai 2026 - 12:35
Najaf na Karbala; Wananchi wa Iraq Washiriki Kwa Wingi katika Hafla ya Kihistoria ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma

Hawza/ Najaf Ashraf leo imeshuhudia ushiriki mkubwa na wa kipekee wa makundi mbalimbali ya wananchi wa Iraq katika hafla ya kihistoria ya mazishi ya Imam Sayyid Ali Khamenei na familia yake ya kishahidi. Hafla hiyo, ambayo leo inaendelea kufanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala, imeambatana na ushiriki mpana wa wananchi kutoka makabila, jamii za kikabila na mikondo mbalimbali ya Iraq.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Najaf Ashraf leo imeshuhudia ushiriki mkubwa na wa kipekee wa makundi mbalimbali ya wananchi wa Iraq katika hafla ya kihistoria ya mazishi ya Imam Sayyid Ali Khamenei na familia yake ya kishahidi. Hafla hiyo, ambayo leo inaendelea kufanyika katika miji mitakatifu ya Najaf na Karbala, imeambatana na ushiriki mpana wa wananchi kutoka makabila, jamii za kikabila na mikondo mbalimbali ya Iraq.

Washiriki, kupitia uwepo wao wa hamasa kubwa na kupaza kaulimbiu za kidini na za kishujaa, huku wakidhihirisha huzuni yao ya kina, wanasisitiza kuendelezwa kwa njia ya Muqawama na kuhifadhi umoja wa Umma wa Kiislamu. Mazingira ya hafla hiyo yamejaa hisia, machozi, dua na mshikamano, na wengi wa waliohudhuria wameuelezea ushiriki wao kuwa ni kufufua ahadi kwa malengo ya Uislamu, Marjaiyya na Muqawama wa Kiislamu.

Kwa mtazamo wa wachambuzi, ushiriki mkubwa wa wananchi wa Iraq katika hafla hii ni alama ya uhusiano wa kina kati ya taifa la Iraq, Marjaiyya ya Kishia, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Mhimili wa Muqawama; uhusiano ambao umejengwa juu ya misingi ya imani za kidini, historia ya pamoja na malengo yanayofanana.

Washiriki walisisitiza kwamba; mkusanyiko huu mkubwa, mbali na kuonesha umoja na mshikamano wa mataifa ya eneo hili, unabeba pia ujumbe ulio wazi kwamba Mhimili wa Muqawama bado unaungwa mkono na wananchi, na kwamba tishio au shinikizo lolote dhidi yake litakabiliwa na umoja na msimamo thabiti wa mataifa ya Kiislamu.

Najaf na Karbala; Wananchi wa Iraq Washiriki Kwa Wingi katika Hafla ya Kihistoria ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma

Sherehe za mazishi zimeendelea tangu usiku uliopita, zikianza kwa mapokezi yaliyofanywa na viongozi wa nchi mbili za Iraq na Iran katika uwanja wa ndege, na baadaye zikaendelea kwa kuhudhuriwa na umati mkubwa wa waombolezaji, usomaji wa Qur'ani Tukufu, usomaji wa nauha na kaulimbiu zinazohamasisha umoja. Hafla hiyo imeonesha mandhari zisizosahaulika za mapenzi, uaminifu na mshikamano wa wananchi wa Iraq kwa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Jeshi la Hashd al-Shaabi la Iraq limetangaza kwamba zaidi ya watu milioni mbili na laki tatu wameshiriki katika mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma huko Najaf Ashraf.

Najaf na Karbala; Wananchi wa Iraq Washiriki Kwa Wingi katika Hafla ya Kihistoria ya Mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Umma

Idadi ya washiriki katika hafla ya mazishi ya mwili mtukufu wa Kiongozi Shahidi wa Umma, Ayatullah al-Udhma Sayyid Ali Khamenei, katika mji wa Najaf Ashraf imevuka watu milioni mbili na laki tatu, na kutokana na kuendelea kuwasili kwa mawimbi ya waombolezaji kutoka sehemu mbalimbali za Iraq, idadi hiyo inaendelea kuongezeka.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha